
Bingwa mara mbili wa Olimpiki wa riadha Usain Bolt amethibitisha kwamba yeye atashiriki katika michezo ya maadhimisho mjini London umbali wa Mita 200 hapo Julai 22 .
Raia huyo wa Jamaica mwenye miaka 29 ambaye ana rekodi ya dunia ya kukimbia mita 200 na sekunde 19 , atakabiliana na Muingereza Adam Gemili.
Naye mfukuza upepo Zharnel Hughes, mshindi namba tano wa mwaka jana katika michuano ya Dunia 200m, naye anatarajia kushiriki katika mbio hizo.