Wananchi wanapewa bili za maji wasiyo tumia -Tulia
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tulia Ackson
ameitaka Wizara ya Maji na Umwagiliaji kushughulikia tatizo la wananchi
kupewa bili za maji huku maji hawapati kwa muda mrefu.
Naibu Spika ameyasema hayo katika kusisitiza swali la Mbunge wa Morogoro
Mjini Abdul-Aziz Abood ambaye amesema Bungeni kwamba wananchi wa
Manispaa ya Morogoro kwa muda wa miezi miwili wamekuwa hawapati maji
lakini wanapelekewa bili ya maji na mamlaka ya maji ili kulipia bili
hizo.
Akijibu Swali hilo Naibu Waziri wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Isack
Kamwele amesema kwamba hii ni mara ya pili kupata malalamiko ya suala
hilo hilo baada ya kupata kero hiyo alipokwenda Manispaa ya Mtwara
Mjini.
''Kuna upotevu wa maji pamoja na wizi wa maji ndiyo unasababisha watu
kupelekewa bili za maji ambazo hawajazitumia''- Amesema Naibu Waziri
Kamwele.
Aidha Naibu Waziri amesema atawasiliana na mamlaka husika kuhakikisha
wanatatua kero hiyo ili mtu alipe maji kulingana na matumizi.
RUDI